CFC Marekani imetoa mwongozo mpya kwa watu waliopata chanjo dhidi ya COVID-19

Dr. Rochelle Walensky, mkurugenzi wa CDC Marekani

“Sayansi inaturuhusu kusema watu waliopata chanjo kamili wanaweza wasivae barakoa, alisema Walensky. Lakini aliongeza kwamba Marekani inahitaji kuwa na wasiwasi juu ya aina mpya ya virusi. Tunahitaji kuwa waangalifu".

Afisa wa afya wa juu Marekani, alisema Jumapili ana matumaini yenye tahadhari kwamba Marekani ipo kwenye njia ya kudhibiti janga la virusi vya Corona.

Ni mapema kutangaza ushindi, Dr. Rochelle Walensky, mkurugenzi wa vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani, alikiambia kipindi cha Fox News Sunday. Tunatakiwa kuendelea kuwa wanyenyekevu.

Lakini aliongeza kusema kwamba, Nina matumaini makubwa kwamba tupo mahala pazuri hivi sasa, ambapo kesi zinaendelea kupungua.

Walensky alitoa tathmini yake pana, ya mapambano ya Marekani dhidi ya virusi vya Corona, siku kadhaa baada ya idara yake kusema watu milioni 123 waliopatiwa chanjo kamili nchini Marekani, kiasi cha theluthi moja ya idadi ya watu, hawahitajiki tena kuvaa barakoa, hatua muhimu katika kuirudisha nchi kwenye hali ya kawaida ya biashara na kijamii.

Mashabiki wa Baseball huko Arizona wakiwa hawana barakoa baada ya muongozo mpya wa CDC

“Sayansi inaturuhusu kusema watu waliopata chanjo kamili wanaweza wasivae barakoa, alisema. Lakini aliongeza kwamba Marekani inahitaji kuwa na wasiwasi juu ya aina mpya ya virusi. Tunahitaji kuwa waangalifu.

Alisema wale ambao wamepatiwa chanjo kamili, hawako katika hatari ya kupata ugonjwa unaopelekea hali mbaya au kulazwa hospitali kutokana na COVID-19. Kama haujapatiwa chanjo, hauko salama”.

Aliwasihi wamarekani ambao hawajapata chanjo kwenda kupata chanjo, akisema asilimia 90 ya nchi hivi sasa, ipo ndani ya kilomita nane, mahala ambapo chanjo zinatolewa. Walensky alisema kutoka chanjo milioni 1.5 hadi milioni 1.2 zinatolewa kila siku nchini Marekani, ikipungua kutoka idadi ya juu zaidi ya milioni tatu.

Lakini mamilioni ya watu kwa sababu moja au nyingine, wanasema hawana nia ya kupata chanjo, wasi wasi ambao unaweza kuzuia mafanikio ya jumla ya nchi katika kupambana na ugonjwa huu unaoambukiza.