Bunge lamthibitisha Waziri Mkuu Ahmed kuendelea na muhula mwengine

Your browser doesn’t support HTML5

Bunge la Ethiopia lilimthibitisha Jumatatu Waziri Mkuu aliyeko madarakani Abiy Ahmed kuendelea na wadhifa huo kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

Wakati Ahmed akiimarisha nguvu zake ndani ya nchi kumekuwa na ongezeko la wasiwasi wa kimataifa kwa serikali yake namna inavyoshughulikia mzozo kaskazini mwa Ethiopia.