Bunge la Marekani limepitisha mswaada utakaofadhili sehemu muhimu za serikali

Jengo la bunge la Marekani

Miongoni mwa vipengele katika mswaada huo ni fedha muhimu za kukabiliana na China katika Pasifiki

Wajumbe wa Bunge la Marekani wamepitisha mswaada Jumapili ambao utafadhili sehemu muhimu za serikali kwa kipindi kilichobaki cha mwaka huu wa fedha ambacho kilianza Oktoba 2023.

Miongoni mwa vipengele katika mswaada huo ni fedha muhimu za kukabiliana na China katika Pasifiki kama sehemu ya makubaliano yaliyosainiwa mwaka jana yaliyoitwa Compacts of Free Association au COFA.

Chini ya mikataba hiyo, Micronesia, Palau na Visiwa vya Marshall vitapokea dola bilioni 7 katika misaada ya kiuchumi kwa zaidi ya miaka 20.

Kwa mabadilishano, Washington itatoa ulinzi wao na inaweza kuinyima China ufikiaji wa maji yao ya eneo, eneo la bahari lenye ukubwa kuliko bara la Marekani. Marekani imekuwa na makubaliano kama hayo na Micronesia na Marshalls tangu mwaka 1986 na Palau tangu 1994. Raia kutoka mataifa haya wanaruhusiwa kusafiri, kuishi na kufanya kazi nchini Marekani siyo kama wahamiaji.