Bunge la Kenya linajadili mswada wa kuondolewa naibu rais madarakani

Naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua

Mswada wa kumshtaki na kutaka kumuondoa madarakani naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua unajadiliwa katika bunge la taifa.

Gachagua anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo uvunjaji wa katiba, ufisadi, unyanyasaji wa wafanyakazi wa serikali, kueneza chuki za kikabila na kudhalilisha serikali anayoitumikia.

Gacgaua anatarajiwa kujibu shutuma dhidi yake saa kumi na moja alasiri hii.

Akizungumza na vyombo vya habari jana jioni, Gachagua aliapa kupinga kabisa madai dhidi yake kwa kila hali.

Amedai kwamba ametengwa katika majukumu ya serikali.

Rais wa Kenya William Ruto alilifuta kazi baraza la mawaziri na kuteua jingine jipya linalohusisha wanasiasa wa upinzani baada ya maadnamano ya nchi nzima kupinga mswada wa fedha mwezi Juni. Watu 50 walifariki katika maandamano hayo.

Gachagua alikuwa amewasilisha kesi mahakamani kulizuia bunge kujadili mswada wa kumshtaki kumwondoa madarakani lakini mahakama kuu ilitupilia mbali ombi hilo.