Viongozi hao kutoka Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini wameweza kufikia kauli moja inayohamasisha biashara ya kimataifa katika mkutano ho wa siku tatu, wakiahidi kupambana na ubinafsi wa kibiashara wakati ambapo kuna vitisho vya ushuru vilivyotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Viongozi hao wamekiri kuwa biashara ya kimataifa inakabiliwa leo na changamoto nyingi kufuatia hatua za Rais wa Marekani Donald Trump kuchukua hatua kadha za kuziwekea ushuru bidhaa muhimu kutoka China na mataifa ya Ulaya.
"Tunatambua kuwa mfumo wa biashara za kimataifa unakabiliwa na changamoto ambazo hazijawahi kutokea. Tunasisitiza umuhimu wa kuwa na uchumi wa dunia uliokuwa wazi," tamko hilo lililokuwa limesainiwa na viongozi watano limesema.