Blinken ziarani Mashariki ya Kati

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Blinken alipokuwa Uturuki

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anatazamiwa kuwasili leo  Ijumaa katika Mashariki ya Kati ikiwa ni ziara yake ya nne katika eneo hilo tangu vita kati ya Israel na Hamas kuanza tarehe 7 Oktoba.

Lengo la safari ya Blinken litakuwa ni juu ya usimamizi wa Gaza baada ya vita wizara ya mambo ya nje ilisema Alhamisi.

Blinken pia atasisitiza wito wa kuongezwa kwa misaada ya kibinadamu huko Gaza, wizara ya mambo ya nje ilisema.

Katika safari ya wiki nzima, Blinken atazuru Israel na Ukingo wa Magharibi, pamoja na Uturuki, Ugiriki, Jordan, Qatar, Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Misri.