Blinken na Rubio wakutana

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, ambaye ataondoka Januari.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, Jumatano amefanya mkutano na Seneta Mrepublikan, Marco Rubio, ambaye ametajwa na Rais mteule Donald Trump kuwa waziri ajaye wa mambo ya nje.

Mkutano huo umefanyika wakati timu ya Trump ikijiandaa kwa mchakato wa kuingia madarakani. “Yalikuwa mazungumzo mazuri, yenye kujenga na muhimu,” naibu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Vedant Patel, aliwaambia wanahabari wakati wa mkutano.

Agosti 2020, China, ilimuwekea vikwazo Rubio, mkosoaji wa muda mrefu wa serikali ya Beijing, pamoja na wengine, wakitaja kile ilichoelezea “tabia mbaya” inayohusiana na maswala ya Hong Kong.

Seneta Rubio ameiambia VOA mapema Disemba kwamba ana uhakika na uwezo wake wa kutafuta suluhu kwa kuwasiliana na Beijing ikiwa atathibitishwa.

Alipoulizwa kama atabaki na msimamo wake wa sera ya mambo ya nje, Rubio amesema rais ndiye anayeweka sera na wao ni watekelezaji.