Blinken:Marekani haina mkakati wa mabadiliko ya utawala nchini Russia

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ka.tika kiako huko Israel Jumapili Machi 27,2022

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Marekani haina mkakati wa mabadiliko ya utawala nchini Russia au pengine popote baada ya Rais Joe Biden siku ya Jumamosi kusema Rais wa Russia Vladimir Putin "hawezi kubaki madarakani."

Biden alitangaza Jumamosi nchini Poland kwamba utetezi wa Magharibi wa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Russia ni muhimu ili kulinda demokrasia duniani kote kwa vizazi vijavyo.

"Jaribio la wakati huu ni mtihani wa wakati wote," Biden alisema katika hotuba iliyotolewa katika kasri ya kifalme alama ya kihistoria ya Warsaw ambayo iliharibiwa katika Vita vya pili vya dunia na kujengwa upya kwa kutumia vifusi katika miaka ya 1970 na 80.

Waziri Blinken katika ziara yake siku ya Jumapili pia alitaka kuwahakikishia washirika wa Israel na Waarabu wanaokutana kwa ajili ya mkutano wa kilele nadra nchini Israel kwamba Washington itaendelea kukabiliana na tishio lolote la Iran wakati akiwa anaipa nafasi diplomasia ya nyuklia na Tehran.

Blinken aliahidi sambamba na kufanya kazi katika kuboresha hali ya Palestina.

Ziara ya Blinken inakuja wakati baadhi ya washirika wa Marekani katika eneo hilo wanatilia shaka dhamira ya utawala wa Rais Joe Biden na kujiandaa kukabiliana na matokeo ya makubaliano ya nyuklia ya Iran na mgogoro wa Ukraine.