Blinken kwenda Haiti na Jamuhuri ya Dominika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, Alhamisi anasafiri Haiti na Jamhuri ya Dominika, ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika mataifa hayo ya Karibian kama mwanadiplomasia mkuu wa Marekani.

Ziara ya Blinken, Port-au-Prince inasisitiza uungwaji mkono wa Marekani kwa Haiti, huku usaidizi wa misaada ya kibinadamu ukitarajiwa wakati nchi hiyo inapambana na ghasia za magenge.

Safari yake ya Santo Domingo inafuatia kuanza kwa muhula wa pili wa Rais wa Jamhuri ya Dominika, Luis Abinader, katikati mwa Agosti.

Afisa mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje amewaambia wanahabari Jumatano kwamba Marekani inatanguliza juhudi na washirika wake wa kimataifa ili kuunda muundo ambao unahakikisha chanzo cha kuaminika cha ufadhili na wafanyikazi kwa misheni ya usalama ya Haiti.