Blinken:Ethiopia inahitaji kufanya maendeleo zaidi katika kutekeleza makubaliano ya amani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akimsalimia Mkuu wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia Daniel Bekele Mratibu Mkazi na Misaada ya Kibinadamu Catherine Sozi, wakati wa mkutano mjini Addis Ababa, Ethiopia Machi 15, 2023. REUTERS

Ethiopia inahitaji kufanya maendeleo zaidi katika kutekeleza makubaliano ya amani na mkoa wa  kaskazini wa Tigray kabla ya uhusiano wake na Marekani kuwa wa kawaida, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani  Antony Blinken alisema.

Akizungumza mjini Addis Ababa Blinken alisema Ethiopia lazima ihakikishe hakuna ukiukwaji mkubwa unaoendelea wa haki za binadamu na kuanzisha mchakato jumuishi na wa kuaminika wa haki ya mpito baada ya mzozo wa miaka miwili wa Tigray.

Kwa uwezo wetu wenyewe wa kusonga mbele katika mazungumzo yetu na Ethiopia ili kujumuisha ushiriki wa kiuchumi pia utasonga mbele Blinken alisema baada ya kukutana na Waziri Mkuu Abiy Ahmed na wengine.

Maelfu ya watu waliuawa katika mzozo wa Tigray kabla ya mkataba wa amani kutiwa saini mwezi Novemba. Mawasiliano benki na huduma nyingine za msingi katika eneo la zaidi ya watu milioni 5 zilikatishwa na hivi karibuni zilianza tena.