Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, yupo Israel kwa mazungumzoJumatano na viongozi wa Israel kuhusu kusitishwa kwa mapigano ya Gaza na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.
Mikutano hiyo na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Waziri wa Ulinzi, Yoav Gallant, na Rais Isaac Herzog, inafanyika siku moja baada ya Blinken, kusema viongozi wa Hamas wametoa majibu yao kuhusu pendekezo hilo.
Blinken aliwaambia waandishi wa habari mjini Doha, Qatar, kwamba Marekani inachunguza kwa umakini majibu hayo, na kwamba wameishirikisha Israel.
Amesisitiza watafanyakazi kwa kadri iwezekanavyo kupata makubaliano na kusonga.
Mjini Washington, Rais wa Marekani Joe Biden, alielezea mwitikio kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Hamas kupewa kipaumbele na kusema mazungumzo yanaendelea.