Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alimaliza safari yake ya mashariki ya kati ili kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina katika ukanda wa Gaza, kwa kusifia uongozi thabiti wa mfalme Abdullah wa Jordan katika kusaidia kupatikana amani.
Michango ya hivi karibuni ya Jordan kusaidia kumaliza mzozo nchini Israel inaonyesha jukumu la kudumu la ufalme kama nguvu ya amnai katika eneo hilo ambayo ni moja ya sababu ya uhusiano wetu wenye nguvu na muhimu sana, Blinken aliwaambia waandishi wa habari baada ya kukutana na mfalme Abdullah huko Amman.
Blinken aliwasili Jordan kituoa cha mwisho ya ziara hiyo kwa mkutano na Mfalme Abdullah ili kuimarisha makubaliano ya usitishaji mapigano. Kuhusu juhudi za kuponya huko Gaza, Blinken alisema jambo la dharura zaidi ni misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza, na hususan maji, usafi wa mazingira, umeme, sote tunapaswa kujumuika pamoja kujibu mahitaji hayo ya haraka. zaidi ya hayo kuijenga tena Gaza.