Blinken aendelea na ziara yake Ukraine

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken aliutembelea mpaka wa Ukraine ambao unalindwa katika vitongoji  vya Kyiv leo hii alipokuwa akiwa katika siku ya mwisho ya ziara ya siku mbili ya kushitukiza.

Ziara hiyo imejumuisha kukabidhi magari yaliyotolewa na Marekani ya mfumo wa kuzuia mashambulizi ambayo ni sehemu ya magari 190 yatakayopelekwa nchini humo katika miezi ijayo.

Waziri Blinken, pia alikutana na timu ya Ukraine inayo fanya kazi kuondoa silaha za Russia, ambazo hazijalipuka katika shamba la mahindi ambayo yangesafirishwa nje ya nchi.

Jumatano Blinken alitangaza msaada mpya wa Marekani wa dola bilioni 1 kwa Ukraine, ambapo dola milioni 175 ni msaada wa ulinzi utakao jumuisha vifa zaidi vya ulinzi, risasi, silaha za kukabiliana na vifaru ikijumuisha risasi za uranium ambazo ziliahidiwa pamoja na vifaru vya Abraham na vifaa vingine.