Biden na Xi Jinping kukutana ana kwa ana mara ya kwanza

Rais wa MarekaniJoe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping

Rais wa Marekani Joe Biden atakutana na mwenzake wa China Xi Jinping kesho jumatatu, ikiwa ni mara ya kwanza viongozi hao wawili kukutana ana kwa ana tangu Biden alipoingia madarakani.

Biden na Xi watakutana wakati kuna wasiwasi kuhusu kisiwa cha Taiwan, vita vya Russia nchini Ukraine na mipango ya utengenezaji silaha za nyuklia ya Korea kaskazini.

Mkutano huo ambao umesubiriwa kwa muda mrefu unakuja wakati uhusiano kati ya Marekani na China umedorora kwa muda wa miongo miwili.

Watakutana kwenye kisiwa cha Bali, Indonesia, kabla ya mkutano wa nchi 20 tajiri zaidi ulimwengu G20.

Mkutano unafanyika baada ya Biden kupata ushindi wa senate huku Xi akiwa ameanza muhula wa tatu madarakani.

Biden na Xi wamewasiliana kwa sim una ua kwa njia ya video mara 5 tangu Biden alipoingia madarakani kama rais, Januari 2021.

Mara ya mwisho wawili hao walikutana ana kwa ana wakati wa utawala wa Barack Obama, Biden akiwa makam rais.