Biden na Trump washinda uchaguzi wa awali Michigan

Rais wa Marekani Joe Biden, na rais wa zamani Donald Trump walishinda katika uchaguzi wa awali wa vyama vyao kwenye jimbo la Michigan Jumanne.

Wote wawili walitarajiwa kushinda, lakini kiwango cha ushindi wao kilikuwa kinafuatiliwa sana kama ya uungwaji mkono kwa wagombea hao wawili katika jimbo hilo muhimu, kabla ya uwezekano wa kupambana tena baada ya ule wa mwaka 2020 ambao Biden alishinda.

Takriban kura zote zilihesabiwa katika uchaguzi wa chama cha Demokrat mapema Jumatano, ambapo rais Biden akiongoza kwa asilimia 81, huku asilimia 13 ya wapiga kura walichagua bila kutangaza mrengo wao.

Michigan ni nyumbani kwa Wamarekani wengi zaidi wenye asili ya kiarabu, na wanapinga hatua ya rais Biden kuunga mkono vita vya Israel huko Gaza dhidi ya wanamgambo wa Hamas.