Biden atoa auheni ya miezi 18 kwa raia wa Hong Kong kuendelea kuishi Marekani

Rais wa Marekani, Joe Biden

Biden alikosoa msako wa miezi 14 kwa demokrasia huko Hong Kong na akasema ilikuwa muhimu kwa  maslahi ya sera za mambo ya nje za Marekani kuruhusu wakaazi wa Hong Kong kukaa na kufanya kazi nchini Marekani

Rais wa Marekani Joe Biden, Alhamis alitoa kile alichokiita “auheni” ya miezi 18 kwa maelfu ya wakazi wa Hong Kong kuendelea kuishi nchini Marekani badala ya kukabiliwa na ukandamizaji kwa kupelekwa katika eneo linalodhibitiwa na China.

Biden alikosoa msako wa miezi 14 kwa demokrasia huko Hong Kong na akasema ilikuwa muhimu kwa maslahi ya sera za mambo ya nje za Marekani, kuruhusu wakaazi wa Hong Kong kukaa na kufanya kazi nchini Marekani. Katika taarifa ya tawi la wizara ya mambo ya nje ya China huko Hong Kong ilisema Biden kwa kutoa kile kinachoitwa hifadhi salama, inajaribu kuipuuza Hong Kong kuipaka matope China, na kujihusisha katika vitendo vya kuharibu ustawi na uthabiti wa jiji kulingana na ripoti ya shirika la habari la Reuters.

Idadi halisi ya watu walioathiriwa na agizo hilo haikujulikana mara moja, lakini afisa mwandamizi wa utawala wa Biden alisema wakaazi wa hong Kong wapatao 330,000 wanaoishi nchini Marekani, wanauwezekano mkubwa wa kuendelea kukaa, isipokuwa watu wowote waliohukumiwa kwa makosa makubwa ya jinai.