Biden atangaza msaada mwingine wa dola milioni 300 kwa Ukraine

  • VOA News

Rais Joe Biden akikutana na Rais wa Poland Andrzej Duda kwenye White House, Machi 12, 2024. Picha ya Reuters

Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne aliwapokea kwenye White House Rais wa Poland Andrzej Duda na waziri mkuu Donald Tusk, huku kukiwa wasiwasi juu ya ufadhili wa baadaye wa Marekani kuisaidia Ukraine kujihami dhidi ya uvamizi wa Russia.

Mkutano huo ulifanyika baada ya utawala wa Biden kutangaza msaada mwingine wa kijeshi kwa Ukraine wa silaha na vifaa vya thamani ya dola milioni 300.

“Haitoshi, Biden alisema kuhusu msaada huo, akiwahimiza wabunge wa chama cha Republican kupitisha msaada wa kigeni ulioidhinishwa na Baraza la Seneti, ambao unajumuisha dola bilioni 60 kwa Ukraine” kabla hali haijawa mbaya.

Rais wa Poland Duda alisema “Uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine” ulionyesha kuwa Marekani inaongoza kwenye suala la usalama. Alitoa kwa mara nyingine wito kwa wanachama wenzake wa NATO kuongeza matumzi yao ya ulinzi hadi asilimia 3 ya pato lao la taifa ili kujihami dhidi ya uvamizi wa Russia.