Biden alionekana katika bustani ya White House akiwa amevalia suti na tai na miwani yake ya kujikinga dhidi ya jua, akionekana ametabasamu.
Biden aliruhusiwa kutoendelea kujitenga baada ya kupimwa mara mbili Jumanne na kukutwa hana virusi vya Covid.
“Nilipata nafuu haraka na ninajisikia vizuri,” Biden amesema.
“Muda wote nilikuwa nimejitenga, niliendelea kufanya kazi, kutekeleza majukumu yangu bila usumbufu wowote. Hii ni taarifa halisi ya wapi tumefikia katika vita dhidi ya Covid 19,” Biden ameongeza.
Biden alikutwa ameambukizwa virusi vya corona Alhamisi iliyopita. Alipata chanjo kamili na chanjo mbili za nyongeza maarufu booster.
Amewahimiza Wamarekani kuendelea kupata chanjo na dozi za nyongeza, maarufu booster, na kuendelea kuwa makini kutokana na ongezeko la aina mpya ya virusi vya Covid ambavyo vinaambukiza kwa haraka.