Amri ya kiutendaji ya Biden inasema wale wanaovuka mpaka kinyume cha sheria kuingia nchini hawatastahiki kupata hifadhi ikiwa tu kuna sababu za msingi kwa nini wanapaswa kuruhusiwa kukaa Marekani.
“Hatua hizi pekee hazitaboresha mfumo wetu wa uhamiaji, lakini zinaweza kusaidia kupata makubaliano kwa kukabiliana vyema na changamoto hii ngumu,” Biden amesema katika hotuba yake kwenye White House.
Kulingana na maafisa wa Marekani, hatua hizo za muda kuhusu kupewa hifadhi zitaanza kutekelezwa wakati idadi ya wastani ya wanaovuka mpaka kila siku itazidi 2,500, na zitasimamishwa idadi hiyo ikishuka chini ya 1,500.
Hatua hizo zinaanza kutekelezwa mara moja.