Biden ampongeza rais mteule wa Argentina, Javier Milei

Rais wa Marekani, Joe Biden, amempongeza rais mteule wa Argentina, Javier Milei, Jumatano, ikulu ya Marekani imesema, siku tatu baada ya mgombea huyo wa siasa kali za kulia kupata ushindi mkubwa wa uchaguzi katika taifa hilo la pili kwa uchumi mkubwa Amerika Kusini.

“Rais Biden, alizungumza na rais mteule wa Argentina, Javier Milei, kwa ajili ya kumpongeza na kujadili umuhimu wa kuendelea na uhusiano wenye tija baina ya mataifa hayo mawili,” taarifa ya White House imesema.

Milei, mchumi mwenye umri wa miaka 53, ameapa kufuta idara nyingi za serikali na aliushinda muungano uliotawala kwa muda mrefu wa Argentina, Jumapili.

Wapiga kura waliacha kuirejesha madarakani serekali kutokana na miongo kadhaa ya kushuka kwa uchumi, na mfumuko wa bei wa kila mwaka ambao kwa sasa umefikiwa kiwango cha asilimia 143.