Benki ya Dunia yasema sheria ya Uganda dhidi ya watu wa LGBTQ inakinzana na maadili ya benki hiyo

Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa duniani nje ya jengo la makao makuu

Timu ya benki ya Dunia  ilisafiri hadi Uganda mara baada ya kupitishwa kwa sheria ya kupitia upya miradi kadhaa ya benki ya maendeleo kimataifa

Benki ya Dunia ilisema Jumanne kwamba sheria ya Uganda dhidi ya watu wa mapenzi ya jinsia moja -LGBTQ, ambayo imelaaniwa na nchi nyingi na Umoja wa Mataifa, inakinzana na maadili ya benki hiyo.

Timu ya benki ya Dunia ilisafiri hadi Uganda mara baada ya kupitishwa kwa sheria ya kupitia upya miradi kadhaa ya benki ya maendeleo kimataifa. Tathmini hiyo ilibaini kuwa hatua za ziada zilihitajika ili kuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya benki ya mazingira na kijamii.

Hatua hizi sasa zilikuwa zinajadiliwa na mamlaka lakini hakuna miradi mipya ya ufadhili wa umma ambayo ingewasilishwa kwenye bodi ya wakurugenzi watendaji wa Benki ya Dunia hadi ufanisi wa hatua za ziada ujaribiwe, Benki ya Dunia ilisema.

Ilisema mifumo ya ufuatiliaji na utatuzi wa malalamiko ya wahusika itaongezwa kwa kiasi kikubwa na kuruhusu benki kuchukua hatua za kurekebisha inapobidi.