Benki ya Dunia kushirikiana na AU katika utoaji wa chanjo za Covid-19

Makao makuu ya Benki kuu

Benki ya dunia imetangaza ushirikiano mpya na Umoja wa Afrika AU, ili kufadhili upatikanaji na usambazaji wa chanjo za Covid-19 kwa takriban watu milioni 400 barani Afrika.

Katika mkutano wa kimitandao wa Zoom, mkuu wa operesheni wa Benki ya dunia Axel van Trotsenburg amesema kuwa benki yake itatoa dola bilioni 12 ili kuhakikisha dozi milioni 400 za chanjo aina ya Johnson & Johnson zitapatikana ikiwa hatua ya kuimarisha mpango wa kupata chanjo kwa Afrika, unaojulikana kama Africa Vaccine Acquisition Task Team, AVATT.

Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya mawaziri wa fedha wa Afrika kufanya kikao na maafisa wa World Bank Group, ili kutadhmini nanma na kuharakisha upelekaji wa chanjo kwa mataifa ya kiafrika ili kuzuia wimbi la tatu la maambukizi ya covid-19.

Mradi huo unasemekana kuwa hatua kubwa katika kusaidia AU, kufikia lengo lake la kutoa asilimia 60 ya chanjo kwa watu wa afrika kufikia 2022.