Benki kuu ya Sudan inachukua hatua za kuleta mabadiliko katika sera za kifedha

Wananchi wa Sudan katika maandamano mjini Khartoum Machi 8,2022.

Benki nchini Sudan na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, yataruhusiwa kuweka kiwago chao cha kubadilisha pesa bila kuingiliwa na benki kuu.

Benki nchini Sudan na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, yataruhusiwa kuweka kiwago chao cha kubadilisha pesa bila kuingiliwa na benki kuu.

Mafisa wa benki kuu nchini humo wamesema hayo bila ya kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu muda ambao hatua hiyo itaanza kutekelezwa.

Kaimu Waziri wa habari amesema kwamba maafisa wa Sudan wameamua kusawazisha kiwango cha ubadilishaji wa pauni ya Sudan.

Hatua hiyo inajiri wiki kadhaa baada ya sarafu ya Sudan kuanza kushuka thamani katika soko lisilo rasmi.

Taarifa ya benki kuu ya Sudan imesema kwamba hatua hiyo inachukuliwa katika hatua za kuleta mabadiliko katika sera za kifedha za nchi hiyo ambazo zitatekelezwa pole pole ili kudhibithi soko la fedha na kuwezesha sekta ya benki kuwa thabithi kabisa.