Uchaguzi wa Jumapili ulikuwa mtihani mkubwa kwa taifa hilo la Afrika Magharibi, ambapo wafuasi wa Talon wanasema alileta maendeleo ya kisiasa na kiuchumi, huku wakosoaji wakieleza kuwa muhula wake ulidhoofisha demokrasia.
Kulikuwa na hali ya utulivu kwenye barabara za mji mkuu wa kiuchumi, Cotonou, masoko na maduka yote yalikuwa yamefungwa, waandishi wa AFP walisema.
Vituo vya kupigia kura vilifungwa saa kumi alasiri kwasaa za huko, lakini muungano wa mashirika ya kiraia ulisema vituo vingi vilifunga kwa kuchelewa.
Uchaguzi wa mwisho wa bunge wa mwaka 2019 uligubikwa na machafuko mabaya, idadi kubwa ya watu ambao hawakupiga kura na kufungwa kwa mtandao wa intaneti, matukio nadra nchini Benin, ambayo awali ilipongezwa kuwa kitovu cha demokrasia eneo la Afrika magharibi.
Upinzani haukuweza kushiriki kwenye uchaguzi wa 2019.