Baraza la wawakilishi Marekani kupiga kura leo dhidi ya Mark Meadows kulidharau bunge

Mark Meadows, mkuu wa utawala wa Rais wa zamani Donald Trump

Meadows ambaye alikuwa Mkuu wa utawala wa Rais wa zamani  Donald Trump alikataa   kutoa ushahidi kuhusu jukumu lake katika kujaribu kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa kushindwa  Trump kwa mwaka  2020

Baraza la Wawakilishi la Marekani linatarajiwa kupiga kura leo Jumanne juu iwapo litapeleka mashtaka kwenye wizara ya sheria dhidi ya Meadows kulidharau Bunge.

Meadows ambaye alikuwa Mkuu wa utawala wa Rais wa zamani Donald Trump alikataa kutoa ushahidi kuhusu jukumu lake katika kujaribu kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa kushindwa Trump kwa mwaka 2020.

Kamati ya bunge inayoundwa na Wademokrat saba na Warepublican wawili walipiga kura kwa kauli moja Jumatatu kupendekeza kwamba Meadows akabiliwe na mashtaka ya uhalifu.

Mark Meadows

Meadows alisema katika mahojiano kwenye mtandao wa Fox News Jumatatu jioni uamuzi wa kamati hiyo ulikuwa wa kusikitisha lakini haushangazi.

Hii inamhusu Donald Trump na hivyo wanamtafuta tena, Meadows alisema. Kabla ya upigaji kura wa kamati hiyo Jumatatu. Mbunge wa chama cha Republican Liz Cheney alielezea ujumbe mfupi wa maandishi uliotumwa kwa Meadows wakati wa shambulio la Januari 6 kwenye majengo ya bunge likiendelea na watu mashuhuri wa vyombo vya habari vya kiconservative na mtoto mmojawapo wa Trump akimtaka Meadows kumshawishi baba yake kufanya zaidi ili kuzuia vitendo vya wafuasi wake.