Azimio hilo lilipitishwa kwa kura tisa za “ndiyo” zilizokuwa zinahitajika na kura 6 zilikuwa za wale waliojizuilia kati ya wajumbe 15 wa Baraza la Usalama.
Balozi wa Marekani Nikki Haley amesema “Marekani haiwezi kuvuta subira tena. Na utawala wa mabavu haukubaliki. Muda mrefu tulitakiwa sote muda mrefu ulopita tuwe tumeshinikiza kupatikana hali bora kwa watu wa Sudan ya Kusini.”
Hata hivyo Baraza la Usalama limechelewesha uamuzi huo kutekelezwa kwa siku 30 ikiwemo kuweka vikwazo vya kusafiri na kukamata mali zao viongozi sita wa Sudan ambao wanatuhumiwa kwa kuzuia kupatikana amani lakini imesema kuwa hatua hiyo bado iko mezani ikisubiri kupitia tena ahadi za vyama hivyo katika kuheshimu kusimamisha uvunjifu wa makubaliano ya kusitisha mapigano.