Baraza hilo jipya litakaloongozwa na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Fathi Bashagha liliidhinishwa na wajumbe 92 kulingana na spika wa bunge Aguila Saleh. Mwanzoni mwa mwezi Februari, Bashagha alitwikwa jukumu la kuunda serikali mpya itakayochukua nafasi ya ile ya Dbeibah ambayo ilibidi kuondoka madarakani baada ya uchaguzi uloahirishwa mwezi wa Disemba. Dbeibah amerudia mara kadhaa kusema kwamba ataacha madaraka baada ya uchaguzi mkuu na kukabidhi utawala kwa seriali iliochaguliwa na raia.
Dbeibah ambaye pia ni tajiri mkubwa wa ujenzi alichaguliwa mwaka mmoja uliyopita ikiwa sehemu ya juhudi za Umoja wa Mataifa za kurejesha utulivu nchini humo kufuatia mapinduzi ya mwaka wa 2011, yaliomuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Moamer Kadhafi.
Jukumu kubwa la Dbeibah lilikuwa ni kuongoza taifa hilo kwenye uchaguzi mwezi Decemba, lakini ukaahirishwa.Baraza la wawakilishi lililochaguliwa mwaka wa 2014 lipo kwenye mji wa mashariki wa Tobruk wakati utawala wa Dbeibah uko kwenye mji wa magharibi wa Tripoli, hali inayoashiria migawanyiko iliyokumba Libya kwa zaid ya muongo mmoja.
Kubuniwa kwa serikali ya Bashagha kunaashiria mawaziri wakuu wawili nchini humo suala ambalo wachambuzi wanasema huenda likazua upya ghasia nchini humo.Umoja wa Mataifa na nchi za magharibi zinamtaka Dbeibah kubaki madarakani hadi kufanyika uchaguzi mpya baadae mwaka huu