Sehemu kubwa ya ulimwengu huchukulia utabiri wa hali ya hewa wa kila siku kuwa wa kawaida. Lakini wengi wa watu bilioni 1.3 barani Afrika wanaishi na ufahamu mdogo wa kile kitakachokuja mbeleni.
Hiyo inaweza kuwa mbaya na ya gharama kubwa pia, na uharibifu unaoendelea katika mabilioni ya dola. Wakati Mkutano wa Kwanza wa Hali ya Hewa barani Afrika ukifunguliwa wiki hii, lakini ukosefu mkubwa wa ukusanyaji wa data ni muhimu.
Bara la Afrika ni kubwa kuliko China, India na Marekani kwa pamoja lakini ina vifaa vya rada 37 tu vya kufuatilia hali ya hewa, kwa mujibu wa hifadhi data ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani.
Amerika Kaskazini inazo rada 291. WMO inasema chini ya asilimia 20 kwa nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara zinatoa huduma ya taarifa za hali ya hewa za uhakika.