Balozi wa Marekani, Japan asikitishwa na kashfa za wanajeshi wa Marekani

Balozi wa Marekani, nchini Japan, Rahm Emanuel ameelezea masikitiko yake Jumamosi kwa kushughulikia kesi mbili za unyanyasaji wa kingono zinazodaiwa kufanywa na wanajeshi wa Marekani, Okinawa.

Kesi hizo zinaonekana kuchochea tena chuki ya uwepo wa wanajeshi wa Marekani kwenye kisiwa hicho cha kimkakati kusini magharibi mwa Japani.

Suala hilo lilizuka mwishoni mwa mwezi uliopita, na kuzua taharuki kutokana na ripoti kwamba wahudumu wawili wa Marekani wamefunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono miezi iliyopita.

Kesi zote mbili ziliripotiwa kwa mara ya kwanza kwenye vyombo vya habari vya ndani mwishoni mwa Juni.

Katika ukamataji wa Machi, mwanajeshi wa kikosi cha anga cha Marekani alishtakiwa kwa utekaji nyara na unyanyasaji wa kijinsia, na mwezi Mei mwanajeshi wa Marekani alikamatwa kwa kujaribu kumbaka na kusababisha jeraha muathirika mwengine.

Taarifa zaidi kuhusu waathiriwa hao hazikutolewa.