Azerbaijan, Jumatatu imesema kwamba imesimamisha kazi katika ubalozi wake nchini Iran, siku kadhaa baada ya mtu mwenye bunduki kuuvamia ubalozi huo na kumuua mlinzi mmoja na kujeruhi wengine wawili.
Iran imesema shambulizi la Ijumaa lilifanywa kwa sababu binafsi, lakini Baku yenyewe imesema ni kitendo cha kigaidi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Azerbaijan, Ayxab Hacizada, aliliambia shirika la habari la AFP, kwamba shughuli katika ubalozi wa Iran zimesimamishwa kwa muda kufuatia kuondolewa kwa wafanyakazi, na familia zao kutoka Iran.
Katika mazungumzo ya simu ya Jumamosi na rais mwenzake wa Iran, Ebrahim Raisi, rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev, amesema ana matarajio ghasia kama hizi za kigaidi zitafanyiwa uchunguzi wa kina.
Polisi wa Tehran wamesema aliyeshambulia alikamatwa na pia ni raia wa Iran alitoa M-Azerbaijan.