Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat leo Jumatatu alitaka kuanza tena mara moja kwa mazungumzo kati ya wanajeshi wa Sudan na raia baada ya vikosi vya usalama kuwashikilia viongozi wakuu katika serikali ya mpito.
Faki alisema katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter kwamba mwenyekiti anatoa wito wa kuanza tena haraka kwa mashauriano kati ya raia na wanajeshi ndani ya muundo wa kisiasa na agizo la kikatiba. Alielezea kusikitishwa na maendeleo huko Sudan ambapo Waziri Mkuu Abdalla Hamdok amekamatwa na pia vikosi vya jeshi viliwafyatulia risasi waandamanaji ambao waliingia mitaani mjini Khartoum kupinga mapinduzi ya Jumatatu.
Alisema mazungumzo na makubaliano ndio njia pekee ya kuokoa kipindi cha mpito cha demokrasia ya Sudan. Faki anazidi kutoa wito wa kuachiliwa kwa viongozi wote wa kisiasa waliokamatwa na kuheshimu vikali haki za binadamu.
AU ilisimamisha uanachama wa Sudan hapo Juni mwaka 2019 baada ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasia wakidai utawala wa kiraia walipouawa nje ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum.