Athari za kimbunga Milton katika jimbo la Florida nchini Marekani

Mafuriko ya maji katika eneo la Siesta Key kutokana na kimbunga Milton kwenye jimbo la Florida. October 10, 2024.

Kimbunga hicho kilipiga Jumatano karibu na Siesta Key katika Kaunti ya Sarasota kikiwa katika kiwango cha kimbunga cha 3

Kimbunga Milton kilikuja na mvua za mafuriko na upepo mkali uliofanya uharibifu katikati na kaskazini mwa Florida siku ya Alhamisi, na kuharibu nyumba na kusababisha vifo vya watu wawili na watu milioni 3 kukosa umeme.

Kimbunga hicho kilipiga Jumatano jioni karibu na Siesta Key katika Kaunti ya Sarasota, kikiwa katika kiwango cha kimbunga cha 3 na upepo mkali wa kilomita 205 kwa saa.

Kwa usiku mzima kilipiga katika jimbo hilo, na kusababisha mamlaka kutangaza dharura za mafuriko, kabla ya kiini cha dhoruba kutokea katika Bahari ya Atlantiki, saa chache kabla ya jua kupambazuka Alhamisi. Kituo cha Taifa cha Kimbunga cha Marekani kimesema eneo la kaskazini mwa Florida linaweza kupata mvua ya sentimita 5 hadi 10 leo Alhamisi wakati kimbunga hicho kikiondoka kutoka jimbo hilo.

St. Petersburg mji ulio kwenye pwani ya magharibi ya Florida karibu na eneo la maporomoko ya ardhi, ulirekodi mvua ya sentimita 41, mara nane ya wastani wa mvua kwa mwezi Oktoba katika jiji.