Annan na Ocampo wakutana na viongozi wa Kenya

  • Abdushakur Aboud

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, kushoto, akizungumza na mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Luis Moreno-Ocampo, kulia, wakati wa mkutano mjini Kampala, Uganda, May 31, 2010.

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan na mwendesha mkuu wa mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu wa KImataifa Luis Moreno Ocampo wamekutana na Rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga mjini Nairobi kutathmini manedeleo yaliyopatikana katika juhudi za mageuzi nchini humo.

Baada ya mkutano huo wa faragha, taarifa ya ikulu inaeleza kwamba Bw Annan aliipongeza serikali kwa kuidhinisha katiba mpya. Akiihimiza nchi hiyo kuendelea mbele na utekelezaji wa katiba ambayo inaleta matumaini makubwa kwa wananchi.

Bw Moreno-Ocampo aliyewasili Nairobi Jumanne alihudhuria mkutano huo na kuitaka serikali kumhakikishia kwamba itaunga mkono kazi za ICC huko Kenya.

Baadae mkutano huo mwendesha mashataka mkuu atahutubia kikao juu ya majadiliano na upatanishi wa kitaifa , kitakacho zungumxzia miaka miwili baadae na mahala walipofika hii leo. Waziri mkuu Odinga atahutubia pia kikao hicho.