Amnesty yasema majeshi ya Ouattara yalitishia makundi ya kikabila baada ya mzozo

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara.

Amnesty international yasema majeshi ya Outtara yalitisha makundi ya kikabila baada ya mzozo.

Shirika moja la kimataifa la haki za binadamu limesema majeshi yanayomuunga mkono rais wa ivory coast Allassane Outtara yaliendelea kuyatisha makundi ya kikabila hata baada ya mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo kusuluhishwa.

Amnesty International ilisema kwenye ripoti yake jana Jumatano kuwa maelfu ya wakimbizi wanaogopa kurudi makwao kwasababu wanakhofia kuwa watashambuliwa.

Taarifa hiyo imesema katika miezi tangu Bw. Outara alipoapishwa makundi ya waasi na wachungaji wa kikabila waliendelea kushambulia makundi ya kikabila ya wale ambao wanaonekana ni wafuaisi wa rais wa zamani Bw. Laurent Bgagbo.