Marekani yaonya kuwa Uganda huenda ikaondolewa AGOA

Serikali ya Marekani imeonya kuwa Uganda huenda ikaondolewa kutoka mpango wa ukuwaji biashara wa Afrika na marekani AGOA, iwapo Kampala,itaendelea kukiuka haki za wananchi wake na kuendelea kuwanyanyasa viongozi wa upinzani.

Gazeti la Uganda la Daily Monitor linaripoti kwamba atika barua iliyoandikiwa waziri wa biashara na Viwanda wa Uganda, Bi Amelia Kyambadde, mshauri wa masuala ya biashara wa rais Obama, Balozi Michael B. G. Froman, alisema kuwa Washington imetambua baadhi ya matukio yanayotia wasi wasi kuhusiana na kujiandikisha tena kwa Uganda, katika AGOA.

Kanuni zilizowekwa na bunge la Marekani ni kwamba kwa nchi kuendelea kufaidika na mpango wa Agoa, ni lazima ionyeshe nia ya kuimarisha demokrasia, kutii sheria na kuwa na uchumi unaofuata kanuni za soko huru. Aidha sheria za AGOA zinahitaji mataifa husika yasikiuke haki za binadamu zianzotambuliwa kimataifa. Froman alisema kuwa seriklai ya Marekani itachunguza kwa makini iwapo Uganda imepiga hatua muhimu katika kuimarisha rekodi yake.