Amadou Fall: BAL inakusudia kuinua programu yake

Rais wa BAL Amadou Gallo Fall.

Msimu wa tatu wa BAL unaendelea huko Senegal.Timu 6 kutoka nchi 4 ziko Dakar zikicheza raundi ya kwanza kutafuta nafasi ya kwenda kwenye fainali zitakazofanyika Kigali.

Timu 12, kanda mbili na nchi tatu.Ligi hii ya BAL inakuvitanisha vilabu bora barani Afrika na washabiki na kuandaa mazingira ya tamasha la michezo linalopita matarajio ya waandaji. Rais wa BAL anasema kila kitu kinakwenda vizuri.

“Matokeo ya jumla ni mazuri sana, nadhani kwa viwango fulani tumevuka hata utabiri au hata malengo ambayo tulikuwa tumejiwekea. Yote yanatokea kwa haraka sana na nadhani ni ushahidi wa msisimko na shauku waliyonayo mashabiki na umma kwa mpira wa kikapu. Na pia kuna vipaji vingi katika bara la Afrika.”alisema Amadou Gallo Fall Rais wa BAL.

BAL inakusudia kuangazia na kuinua programu yake. Pia inakusudia kuwashirikisha wachezaji wachanga wa Chuo cha NBA. BAL inataka wachezaji wawe na uzoefu mkubwa huku wakipata matokeo ya kuridhisha.

“Wasiwasi wetu wa kimsingi unabaki kuwa ubora wa mchezo umeboreshwa sana na nadhani kwa kupitia Elevate mwaka jana tuliona baadhi ya vijana hawa wakianza. Babacar Sane ambaye sasa anatia saini mkataba na timu ya G-League Ignate. Pia wapo wengine ambao wamekwenda kujiunga na vyuo vikuu vikubwa vya Marekani, lakini wengi zaidi wamebaki na kuendelea na mafunzo yao katika ngazi ya NBA Academy na wamerejea mwaka huu kwenye BAL” aliongeza Fall

BAL inaona ni muhimu kwamba wachezaji wachanga wa mpira wa kikapu wa Kiafrika kufanikiwa wakiwa wamebaki barani Afrika. Ligi hiyo inataka kujidhihirisha kama mshiriki mkuu katika uchumi wa Afrika.

“Tasnia hii itakuza na kuhamasisha vijana kutafuta shughuli nyingine ambazo hawajazifikiria hadi sasa na zitawapeleka kwenye ajira kwani kwetu mwanzo tunahitaji utaalamu na utaalamu huu tunauleta kwa kiasi fulani kutoka nje. Lakini baada ya muda ni kuwa na utaalamu huu hapa katika ngazi ya kanda hii” aliongeza Fall.