Aliyekuwa waziri mkuu na mawaziri wengine 3 washitakiwa kwa ufisadi Guinea

Kiongozi wa kijeshi nchini Guinea Mamadi Doumbouya akiapishwa kama rais wa serikali ya mpito mjini Conakry, Guinea Oct. 1, 2021. PICHA: REUTERS

Aliyekuwa waziri mkuu wa Guinea Ibrahima Kassory na mawaziri watatu wa zamani, wanatarajiwa kufunguliwa kesi mahakamani mjini Conakry, ya matumizi mabaya ya pesa za uma.

Watuhumiwa walikamatwa wiki iliyopita.
Kassory alikamatwa pamoja na aliyekuwa waziri wa ulinzani Mohamed Diane, waziri wa mazingira Oye Guilavogui na aliyekuwa waziri wa mafuta Zakaria Coulibaly.

Watafunguliwa mashtaka ya kuharibu uchumi wa Guinea na makossa mengine ya kifedha, baada ya kuhojiwa kwa mda wa siku tatu.

Kassory alikuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 2018 hadi Alpha Conde alipopinduliwa na jeshi mwezi Septemba mwaka uliopita.

Utawala wa kijeshi umeapa kupambana na ufisadi na wala sio kuwaandamana watu mashuhuri waliokuwa katika serikali iliyoondoka madarakani.