Aliyekuwa Rais wa mpito wa Bolivia Jeanine Áñez alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela Ijumaa kwa mashtaka yanayohusishwa na kutwaa madaraka mwaka 2019 huku kukiwa na maandamano ya vurugu yaliyosababisha kujiuzulu na kufukuzwa kwenda kuishi uhamishoni kwa mtangulizi wake, Evo Morales.
Áñez alikutwa na hatia na mahakama kwa kutotimiza wajibu wake na kutenda kinyume na katiba alipojitangaza kuwa rais katika kile ambacho Morales na chama chake wamekiita mapinduzi.
Wafuasi wa Áñez wanakanusha kuwa yalikuwa mapinduzi, wakisema madai ya matumizi mabaya ya madaraka ya Morales yalisababisha ghasia halali mitaani. Kuondolewa kwa rais wa kwanza wa Bolivia na makamu wake kuliunda ombwe la mamlaka ambalo lilimruhusu Áñez kutwaa urais wa muda kama rais wa pili wa Seneti, wanadai. Upande wa utetezi ulisema atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.