Aliyekuwa kiongozi wa waasi DRC Roger Lumbala anazuiliwa Ufaransa

Roger Lumbala

Ufaransa imeanzisha uchunguzi kuhusu aliyekuwa kiongozi wa waasi wa M23 nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Roger Lumbala.

Lumbala anashutumiwa kwa kushiriki katika kupanga uhalifu wa kibinadamu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002.

Uchunguzi dhidi yake unafanyika baada ya kukamatwa jumamosi.

Anshutumiwa kwa kupanga mapigano kati ya makabila ya Nande na Twa, kaskazini mashariki mwa Ituri.

Umoja wa mataifa ulishutumu chama chake Lumbala cha demokrasia taifa – RCD-N, kwa ukiukwaji wa haki za kibinadamu.

Lumbala aliwahi kuwa waziri na baadaye mbunge wa upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.