Al-Shabab wadai kuuwa 61 katika shambulizi Somalia

Wapiganaji wa al-Shabab

Kikundi cha al-Shabab chenye msimamo mkali kimedai kuwa kimehusika na mauaji ya wanajeshi wasiopungua 61.

Wamesema wamefanikisha hilo kufuatia shambulizi lao kwenye kituo cha kijeshi nchini Puntland ambayo inajitawala yenyewe baada ya kujitenga na Somalia.

Kikundi cha al-Qaida kimedai kuhusika na shambulizi hilo la Alhamisi asubuhi katika kituo cha jeshi huko Af Urur, karibu na kituo cha kibiashara cha Bossaso.

Kikundi cha usalama cha SITE, kinachofuatilia makundi yenye misimamo mikali, kimesema al-Shabab ilieleza kuhusika kwake kupitia shirika lake la habari Shahada News Agency.

Kikundi hicho pia kimesema kuwa kimekamata kiwango kikubwa cha silaha na risasi na zaidi ya dazeni moja ya magari ya kijeshi.

Puntland iliyoko upande wa kaskazini mwa Somalia pia kinakabiliwa na tishio kubwa la wapiganaji wakikundi cha Islamic State waliojitenga na al-Shabab.