Watu watano wamefariki kutokana na shambulizi lililofanywa na kundi la kigaidi la al-shabaab katika mji mkuu wa Mogadishu.
Wizara ya habari ya Somalia imesema kwamba kundi la al-shabaab, lenye uhusiano na kundi la al-Qaeda, lilitekeleza shambulizi hilo jana jumapili.
Walilipua bomu kabla ya kuingia kwa nyumba ambazo meya wa Mogadishu anaishi.
Wizara ya habari ya Somalia imesema kwamba washambuliaji sita waliuawa katika shambulizi hilo la adhuhuri, na kufikia saa kumi na mbili jioni, hali ilikuwa imerejea kuwa tulivu.
Wizara ya habari imesemwa kwamba raia watano walifariki, huku msemajo wa polisi akisema kwamba idadi ya vifo imefikia watu sita, huku mkuu wa huduma za dharura akisema kwamba walisafirisha miili ya raia wanane.