Afrika magharibi ni mwenyeji wa mikutano miwili ya marais wikiendi hii

Ramani ya Niger ikionyesha mji wake mkuu Niamey pamoja na nchi zilizo karibu nazo.

Mkutano wa leo Jumamosi nchini Niger wa muungano wa mataifa ya Sahel na mwingine Jumapili nchini Nigeria wa ECOWAS

Afrika Magharibi iliyogawanyika itakuwa mwenyeji wa mikutano miwili ya marais wikiendi hii, mmoja nchini Niger kati ya viongozi wa utawala wa kijeshi wa kanda ya Sahel ukifuatiwa na mwingine nchini Nigeria kesho Jumapili na viongozi wa jumuiya pana ya uchumi.

Mkutano wa leo Jumamosi katika mji mkuu wa Niger Niamey, utakuwa wa kwanza kati ya viongozi wa kijeshi wa jumuiya mpya ya kikanda, muungano wa mataifa ya Sahel (AES).

Niger na nchi zilizo karibu nazo.

Mali, Burkina Faso na Niger zilianzisha mkataba wa ulinzi wa pamoja mwezi Septemba, na kuondoka katika jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) mwezi Januari. Kujiondoa kwao ECOWAS kulichochewa kwa sehemu na madai yao kwamba Paris ilikuwa ikiendesha umoja huo, na kutotoa msaada wa kutosha katika juhudi za kupambana na jihadi.

Kuondoka huko kumekuja wakati ambapo mataifa hayo matatu yalipohama kutoka kwa mtawala wao wa zamani wa kikoloni Ufaransa na kuwafukuza wanajeshi wa Ufaransa wanaopinga jihadi na kugeukia kile wanachokiita washirika wao wa dhati- Russia, Uturuki na Iran.