Waziri wa Afya Zwelini Mkhize alitangaza Jumamosi usiku idadi hiyo mpya ambayo ndio kubwa zaidi nchi humo kwa siku.
Vyanzo vya habari vimeeleza maambukizo hayo hivi sasa ni zaidi ya asilimia 50 ya maambukizo yote yaliyoripotiwa katika nchi 54 za Afrika.
Afrika Kusini sasa ina jumla ya watu 503,000 wenye kuuguwa ugonjwa wa COVID-19.
Takwimu zinaonyesha watu 8,153 wamekufa kutokana na COVID -19 nchini humo. Afrika Kusini ina idadi ya watu milioni 58.
Kwa mujibu wa ripoti za tafiti mbalimbali duniani taifa hilo hivi sasa linashika nafasi ya tano duniani kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya maambukizo.
Nchi ambazo zina idadi kubwa ya maambukizo duniani ni Marekani, Brazil, Russia na India.