Afrika Kusini inashudia ongezeko la maambukizo ya COVID-19 ambapo wagonjwa wengi hivi sasa ni wale wanaoambukizwa na virusi viupya vya Omicron.
Mwanabiolojia wa Taasisi ya Kitaifa ya Magonjwa ya Kuambukiza Profesa Anne von Gottberg amesema hii kwamba maambukizo yanafanyika kwa kasi kuliko ilivyowahi kushuhudiwa hapo awali. .
Akizungumza kwenye mkutano kwa njia ya mtandao ulioandaliwa na Shirika la Afya Ulimwenguni.-WHO hii Profesa Gotterb amesema hapo awali maambukizo yalikuwa yanaweza kulindwa dhidi ya Delta lakini sasa anasema inaonekana hiyo haiwezekani kwa upande wa Omicron,
Wakati huo huo mkurugenzi wa kikanda wa masuala ya dharura wa WHO Salam Gueye anasema Shirika lake linatuma timu ya kudhibiti magonjwa katika jimbo la Gauteng la Afrika Kusini, kwenye kitovu cha mlipuko wa aina mpya ya ugonjwa wa Omicron, ili kusaidia uchunguzi na ufuatiliaji wa mawasiliano, lilisema Alhamisi.
Anasema WHO inatoa pia msaada wa kiufundi kuimarisha uzalishaji na usambazaji wa gesi ya Oxygen nchini Botswana ambako Omicorn imegundukliwa pia.