Serikali ya Afrika Kusini ilisema Ijumaa kuwa itaingiza msaada mpya wa dola bilioni 2.5 kwa shirika linalokabiliwa na hali ngumu ya usafirishaji la Transnet huku ikikabiliana na mrundikano mkubwa wa mizigo bandarini.
Maelfu ya makontena yamekwama baharini karibu na bandari ya Durban kwa sababu ya kuharibika kwa vifaa na meli nyingi sasa zinakwenda katika nchi nyingine, maafisa walisema.
Idara ya Hazina ya Kitaifa ilisema kuwa msaada wa bilioni 47 utaisaidia kampuni hiyo ambayo ilisema ina jukumu kuu katika uchumi kukidhi majukumu ya deni yanayokuja.
Shirika limekumbwa na changamoto kubwa za kiutendaji, kifedha na kiutawala katika siku za hivi karibuni na linajitahidi kutekeleza jukumu hili la kimkakati,idara ya Hazina ilisema.