Kati ya sera hizo ni pamoja na kutengeneza vituo vya kushughulikia wanao omba hifadhi ya ukimbizi kupitia mpaka wa nchi hiyo.
Hii inaashiria mwisho wa uhakika wa kupata uraia baada ya kuwa mkazi wa muda mrefu nchini humo. Pia kuanzishwa kwa utaratibu wa pointi unaokusudia kuwavutia wahamiaji wenye ujuzi na kuondoa baadhi ya masharti ya viza kwa raia wa Kiafrika.
Pendekezo la mabadiliko hayo limekuja wakati nchi imegubikwa na chuki na vitendo vya uvunjifu wa sheria dhidi ya wahamiaji wa Kiafrika, hali kukiwa na maoni kwamba“ hilo sio jambo linalopendeza na wala haiwezekani kuzuia uhamiaji wa kimataifa.”
Waziri wa Mambo ya Ndani Malusi Gigaba amesema pendekezo hilo, ambalo litapelekwa mbele ya bunge wiki ijayo, linakusudia kuweka uwiano unaoridhisha kati ya kuwakaribisha wahamiaji wengi kutoka nchi za Afrika na kuhakikisha usalama wa taifa.
Sera hiyo mpya imekuja wakati kumekuwa na wimbi la uvunjifu wa amani katika wiki za karibuni dhidi ya wahamiaji wa Kiafrika, ambao waandamanaji wanaochukua sheria mikononi mwao wanawatuhumu wahamiaji kwamba wamechukua kazi zao na rasilmali chache kutoka kwa wananchi wa Afrika Kusini.
Mwaka jana, Idara ya Mambo ya Nje ilisema kuwa watu milioni 16 waliwasili Afrika Kusini. Wengi kati yao wametoka nchi za jirani zikiwemo Lesotho, Zimbabwe, Mozambique, Swaziland na Botswana. Serikali ilisajili kuwasili kwa zaidi ya Wamarekani 400,000 na zaidi ya raia wa Uingereza 560,000.
Mwaka huo huo, maafisa wa uhamiaji waliwasafarisha zaidi ya watu 23,000, wengi wao kutoka Mozambique, Zimbabwe, Lesotho, Swaziland na Malawi.
Tony Elumelu, mkurugenzi wa Tume ya Uhuru wa Watu Kutembea (nchi moja hadi nyingine) kwa jamii ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi, amesema sera iliyo pendekezwa na Afrika Kusini itafanya kazi vizuri kutokana na hali ya wahamiaji wa kimataifa wanaopita nchini.
Wanaharakati wa haki za binadamu wameeleza wasiwasi wao juu ya pendekezo hilo. Jacob van Garderen, mkurugenzi wa taifa wa mawakili wa haki za binadamu, amesema pendekezo hilo juu ya wanao omba hifadhi ya ukimbizi wana wasiwasi.
Gigaba atawasilisha pendekezo hilo kwenye Baraza la Mawaziri la Afrika Kusini wiki ijayo. Amesema anamategemeo makubwa kwamba itapitishwa na mabadiliko hayo yataanza kutumika mwaka 2018.