Afrika Kusini yafikia maambukizi 8,500 ya COVID-19 saa 24 zilizopita

Mkurugenzi wa afya San Francisco Dkt Grant Colfax aeleza kugunduliwa kwa maambukizi ya kwanza ya omicron wakati Meya London Breed, kulia, akisikiliza City Hall in San Francisco, California, Dec. 1, 2021.

Virusi vya Omicron vinavyosababisha COVID-19 sasa vimetawala Afrika Kusini  na vinasababisha ongezeko la maambukizi mapya.

Taasisi ya taifa ya magonjwa ya kuambukiza imesema zaidi ya asilimia 70 ya maambukizi ya virusi yameongezeka mwezi uliopitana kutokana na virusi vipya. afrika kusini imeandikisha kesi mpya za COVID 19, 8,500 katika saa 24 zilizopita.

Kumekuwa na ongezeko endelevu la maambukizi mapya ya COVID-19 katika maeneo mengi ya nchi. Kwa mujibu wa wizara ya afya ya nchi hiyo ongezeko hilo limeripotiwa katika majimbo saba ya nchi.

Maambukizi mapya yanatarajiwa kuongezeka katika wimbi la nne la sasa Afrika Kusini. Wizara ya afya imesema kumekuwa na ongezeko kidogo kwa wagonjwa kulazwa hospitali.

Taasisi ya taifa ya magonjwa ya kuambukiza imesema watu wengi waliolazwa katika hospitali hawajapokea chanjo dhidi ya corona.

Maafisa wa marekani jana walisema Kesi ya kwanza imethibitishwa kutoka kwa mtu mmoja kwenye jimbo la California.

Dkt Anthony Fauci mtaalamu wa juu wa magonjwa ya kuambukiza na mshauri wa afya wa rais Joe Biden amewaambia waandishi wa habari mtu huyo alikuwa amerejea Marekani kutoka safarini Afrika Kusini Novemba 22 na alipimwa Jumatatu na kukutwa na virusi hivyo.