Afrika Kusini: Rais Cyril Ramaphosa aapa kukabiliana na 'pesa chafu'

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akitoa hotuba kuhusu hali ya taifa mjini Cape Town, Februari 9, 2023

Rais Cyril Ramaphosa Jumatatu amesema Afrika Kusini itatumia fursa kukabiliana na pesa chafu baada ya nchi hiyo kuwekwa kwenye orodha ya waangalizi wa uhalifu wa kifedha.

Taasisi ya kimataifa inayofuatilia masuala ya fedha, Financial Action Task Force (FATF), siku ya Ijumaa ilisema kuwa imeiweka Afrika Kusini kwenye orodha yake inayojulikana kama ‘grey list’, kwa kuongeza ufuatiliaji juu ya mapungufu katika kupambana na utakatishaji wa fedha, ufadhili wa ugaidi na ufadhili usio wa wazi.

“Hali inatia wasiwasi lakini sio mbaya kama baadhi ya watu wanavyodai,” Ramaphosa amesema.

“Misingi imewekwa na tunajua kile tunachohitaji kufanya ili kuondoka kwenye orodha hiyo”, ameongeza, na kusisitiza kuwa na dhamira ya kutekeleza jambo hilo haraka iwezekanavyo.