Pretoria imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya kidiplomasia tangu mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) ilipotoa hati ya kumkamata Putin, ambaye anatarajiwa kufanya ziara nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mkutano wa nchi wanachama wa BRICS mwezi Agosti.
Jumanne, chama cha Democratic Alliance kimesema kimeanzisha mchakato wa kuwasilisha ombi mahakamani kuhakikisha serikali inamkamata kiongozi huyo wa Russia na kumkabidhi kwa ICC ikiwa Rais Putin atafika nchini Afrika Kusini.
“Hatua hii ya awali ya kwenda mahakamani inalenga kuhakikisha kuwa Afrika Kusini inatekeleza wajibu wake,” Glynnis Breytenbach anayehusika na masuala ya sheria kwenye chama cha Democratic Alliance amesema katika taarifa.
Afrika Kusini ambayo ni mwanachama wa ICC, ina uhusiano wa karibu wa kidiplomasia na Moscow inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa BRICS ambao unajumuisha nchi za Brazil, Russia, India, China, na Afrika Kusini.