Mataifa ya Afrika yatafuta suluhisho kwa athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Athari za mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika

Wassila Thiaw mkuu wa kitengo cha Afrika, kutoka idara ya kitaifa ya kimarekani ya bahari na anga, anasema mvua nyingi zaidi zitalea mafuriko kwa baadhi ya maeneo ya Somalia, Kenya na Tanzania katika kipindi cha miezi miwili ijayo.

Your browser doesn’t support HTML5

africa climate change

Mataifa kote barani Afrika yanatazamia mkutano wa umoja mataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa huko mjini Paris, haraka kutafuta masuluhusho la kugeuza athari za ongezeko la jotojoto kwenye mifumo ya bahari kote duniani.

Katika baadhi ya sehemu za kusini mwa Afrika, mkusanyiko wa mawimbi ya joto na ukame, kutokana na mfumo wa hali ya hewa ujulikanao kama El Nino, umeathiri Zimbabwe na Afrika kusini.

Mkuu wa jumuiya ya wazimbabwe nchini Afrika kusini, Ngqabutho Mabhena, anasema wana ukame mkubwa, ukosefu wa maji ya kunywa na ukosefu wa mvua.

Anasema tunakosa ardhi ya malisho ya mifugo, sasa, mifugo inakufa kwa wingi. Haya yote ni athari za mabadiliko ya hali ya hewa nchini Zimbabwe.

Nako nchini Afrika kusini, athari za mabadiliko ya hali ya hewa pia zimekuwa mbaya. Taifa hilo haraka linapungukiwa na maji, na idadi kadhaa za majimbo yake tayari yametangazwa kuwa maeneo ya ukame, na kutishia usalama wa chakula nchini humo.

Waziri wa maji na mazingira wa Afrika kusini, Edna Molewa, anasema serikali yake inafanya kila iwezacho kukabiliana na ongezeko la joto duniani, ikiwa ni pamoja na kutazamia athari za muda mfupi na mrefu za mabadiliko ya hali ya hewa nchini humo.

Anasema serikali inashughulikia kwa njia nyingi tofauti. Anasema tuna sera kabambe za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na pia tunatazamia masuala ya utafiti.

Viwango vya hali ya hewa duniani mwaka 2015, vinatarajiwa kuwa vya joto zaidi kuwahi kurekodiwa kwa mujibu wa shirika la dunia la hali ya hewa la umoja mataifa.

Linasema athari za mabadiliko ya hali ya hewa yamepelekea kuongozeka kwa joto takriban degree moja ya celcius juu kuliko enzi ya viwanda.

Umoja mataifa unataka hali ya joto duniani isiongezeke zaidi ya degree celcius mbili.

Nchini Burundi, mvua nyingi zisizo za kawaida zimenyesha kote nchini, na kusababisha maporomoko ya ardhi ambayo yalipelekea vifo na uharibifu kwa nyumba na miundo mbinu.

Taifa jengine la kiafrika linalokabiliwa na mvua nyingi ni Nigeria. Ben Bem Goong, mkuu wa wizara ya mazingira nchini humo, anasema msimu wa mvuo umekuja mapema zaidi na ulikuwa na nguvu Zaidi.

Alhassan Mohammed mwanasaynsi wa mazingira katika chuo kikuu cha Abuja, anasema athari imekuwa mbaya sana kwa wale wanojishughulisha na sekta ya kilimo.

Wassila Thiaw mkuu wa kitengo cha Afrika, kutoka idara ya kitaifa ya kimarekani ya bahari na anga, anasema mvua nyingi zaidi zitalea mafuriko kwa baadhi ya maeneo ya Somalia, Kenya na Tanzania katika kipindi cha miezi miwili ijayo.